Sunday, June 5, 2011

Irresponsibility of Some of Tanzania's Media

In Tanzania we have been enjoying free of speech unparalleled by many countries in this planet. However, there has been a trend of gross irresponsibility by our journalists and the public have been constantly fed by ridiculously articles. I ran into this piece published by RAIA MWEMA on June 1st, 2010, that demonstrated the sheer negligence of professionalism and ethics of fine journalism. Somebody, should get Jenerali Ulimwengu (whom I greatly respect) to read the articles that his affiliated newspaper is publishing.

Here is the piece and some comments that I inserted.

Kikwete na Porojo za Kujivua Gamba

Na Mwandishi Maalumu (You can not publish article with this amount of allegations without revealing the author)

NI vigumu kuamini kwamba rais wa nchi anaweza kuhusika na mchezo mchafu kama huu wa kuwabagua wananchi wake kwa misingi ya dini zao, lakini matukio ya hivi karibuni yanathibitisha hilo.( How? Show us the causality)

Baada ya uchaguzi mwaka jana na hasa tukio la Arusha la Watanzania kupigwa na polisi kwenye maandamano ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), na kisha harufu ya udini kuibuka, baadhi ya Waislamu wachache wenye mtazamo mkali walianza kuzunguka nchi nzima wakitoa mahubiri ya chuki. (Dates, Names, what exactly did they say? At least have a source)
Mkutano mmoja ulifanyika kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam na inadaiwa ulipata baraka za Kikwete (How can we believe u?). Baadhi ya mikutano hiyo ilijadili masuala tata, na baadhi ikaibuka hata na mapendekezo ya ajabu ukiachilia yale ya muda mrefu kama vile kudai Mahakama ya Kadhi na Tanzania kuingia kwenye Jumuiya ya Kiislamu Duniani (OIC).
Madai mengine yalihusu malalamiko kwamba Wakristo wamekuwa wakipendelewa tangu enzi za ukoloni na kwamba ingawa Waislamu ni wengi zaidi Tanzania, lakini hawana nafasi nyingi za madaraka.

Madai mengine yaliyotolewa ni kwamba Wakristo wana shule na mahospitali lakini Waislamu hawana, na kwamba serikali hutoa fedha kuzisaidia hospitali za Wakristo na walimu wa kufundisha shule za Wakristo, lakini Waislamu wanaachwa hivi hivi tu.

Baadhi walifikia hata hatua ya kumlaani Mwalimu Nyerere na kusema kwamba hastahili kuitwa Baba wa Taifa; bali anastahili kuitwa Baba wa Kanisa Katoliki. Baadhi yao, akiwemo kigogo wetu, hawamwiti Mwalimu Nyerere kwa hadhi yake iliyozoeleka ya Baba wa Taifa, na badala yake humwita Mzee Nyerere.( We need dates of the events, and names of attendees. At least a background interview. You can’t just throw allegations with NO evidence. WaTanzania sio wajinga hivyo).

Kwa ufupi, kuna imani kubwa miongoni mwa Watanzania kwamba utawala wa Rais Kikwete unalea udini (Do u have a scientific poll to back this up? ), na asipokuwa makini nyufa hii yenye msingi wa kidini inaweza kupanuka na kuutia dosari umoja wa kitaifa tulionao ambao misingi yake si udini.

Geresha ya kujivua gamba

Pamoja na kubadili safu ya uongozi mjini Dodoma, CCM pia ilitangaza kwamba wanachama wake watatu wanaotuhumiwa kwa ufisadi wajiondoe wenyewe; la sivyo wataondolewa kwa nguvu. Wanachama hao wanatajwa kuwa ni Waziri Mkuu aliyejiuzulu, Edward Lowassa, na wabunge wawili, Andrew Chenge na Rostam Aziz. Ni kweli matajiri hawa hawapendwi na Watanzania wengi isipokuwa pengine wa majimboni mwao tu.

Lakini pia watu hawa watatu wana sifa nyingine: Kwamba ndio tishio pekee na la kweli dhidi ya mpango wa Kikwete wa kusaka mgombea urais wa mwaka 2015 ambaye ni Mwislamu (This is unprecedented. You are accusing the head of state of being mdini, but you are not telling us readers how u have arrived to this conclusion?)Wanaotaka kumweka Lowassa kwenye urais mwaka 2015, si tu wanakwamishwa na tuhuma hizi zinazomwandama na hatihati hii ya kung’olewa CCM, lakini pia wanakwazwa na Kikwete mwenyewe. Inadaiwa kwamba, kwenye mbio za urais za 2015, tatizo la Kikwete kuhusu Lowassa si kwamba anakabiliwa na tuhuma za ufisadi; bali kwamba si Mwislamu. (You are supposed to quote your sources on this sentence. How can we believe u?)

Kundi hili la kina Lowassa inaaminika lina urafiki wa karibu na Makamba ambaye inadaiwa kuwa agenda yake kubwa kwa mwaka 2015 haikuwa udini; licha ya kuwa naye amesikika mara kadhaa akilumbana na maaskofu (Disagreeing with Maaskofu does not make one Mdini); bali yeye (Makamba) ana ndoto ya mwanae (January) aje kuachiwa urais mwaka 2025 na kundi hili(Now you can read people’s dreams too? How can a respectable news as Raia Mwema publish this nonsense?). Makamba hutamba kwamba mwanae anafaa kuwa kiongozi, na hakuna ubishi kwamba alihakikisha mwanae anapata ubunge, uenyekiti wa kamati ya Bunge, na kisha kuingia kwenye Sekretarieti ya CCM.

Aidha, mtoto huyo wa Makamba pia anaelezwa kuwemo kwenye kundi linalowaunga mkono watuhumiwa hawa wa ufisadi ambalo lina idadi kubwa ya wabunge na viongozi wa CCM wa ngazi za wilaya, mikoa na taifa. Hii ndiyo sababu tangu CCM ilipoanza kushambulia mafisadi hadharani, yeye amepotea jukwaani!( Have u reach to him and ask for him to comment? That is how professional journalists operates. You just made up your own reasons as if January do not exist.)

Kimsingi, kuna kutofautiana kati ya Makamba na Kikwete kuhusiana na nani awe rais mwaka 2015 na kuhusu nini wafanyiwe hawa watuhumiwa wa ufisadi. Hivyo; tangazo la kujivua gamba pamoja na kutajwa kwa watuhumiwa hao ambao Kikwete mwenyewe aliwapigia kampeni mwaka jana kwenye uchaguzi wa wabunge, ni geresha tu. Ukweli ni kwamba Kikwete alikuwa anaunda timu itakayomrithi mwaka 2015.

Kimsingi, hadi sasa Kikwete ameshawaacha ‘wabaya’ wake wote nje ya Kamati Kuu ambao ‘dhambi’ yao kuu ni kuutaka urais wa mwaka 2015. Watu hao ni pamoja na Membe na Andrew Chenge ambaye anamtaka Lowassa. Kwa ufupi, janja hii ya Mwenyekiti Kikwete ya “kujivua gamba” ililenga katika kuwaengua wale wote wanaoweza kumsumbua kwenye suala la urais wa mwaka 2015; ingawa pia ni kweli kwamba ukiuangalia juujuu utaona kuwa mpango huo wa “CCM kujivua gamba” unalenga katika kupunguza nguvu za CHADEMA kwa kuirejeshea CCM mvuto wake wa zamani.

Vyovyote vile; hakuna ushujaa wala maamuzi magumu yaliyofanyika Dodoma. Ulikuwa ni ‘usanii’ tu, na ndiyo sababu hakuna kiongozi wa CCM anayepigia kelele kung’olewa chamani mafisadi zaidi ya kijana Nape na Katibu Mkuu mpya, Wilson Mukama ambao, hata hivyo, nao wamefungwa “gavana” hivi karibuni kuhusu kulipigia debe suala hilo. Hata Chiligati aliyejitokeza mwanzoni kuhubiri nia ya kuwavua uongozi wa CCM kina Lowassa, Rostam Aziz na Andrew Chenge, sasa naye ameingia mitini!( Sources?)

Kauli ya Joseph Butiku

Labda nigusie pia kidogo kuhusu malalamiko ya Joseph Butiku aliyoyatoa katika mahojiano na gazeti la Raia Mwema, hivi karibuni, kwamba viongozi wa CCM wamemwachia Mwenyekiti Kikwete mzigo wa kupambana na mafisadi.
Mimi nadhani madai hayo ya Butiku ameyatoa bila kujua ukweli wa mambo. CCM haiko kwenye mapambano na mafisadi; bali Mwenyekiti Kikwete ndiye anapambana na maadui zake kwenye kinyang’anyiro cha kutafuta mrithi wake kwenye Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015; ila tu amepata bahati kwamba watu hao hao ndio wanaolalamikiwa kwa ufisadi. Ni bahati tu ya mtende iliyotoa fursa ya ‘usanii’ huu kuchezwa! (Last election was a referendum on corruption more than anything. But you seem to disagree. You argument is “luck”. You know we can reach conclusion to every issue by attributing it on luck)

Aidha, kelele za CCM kupitia kwa Nape kwamba kuna vyombo vya habari, viongozi wa Upinzani na viongozi wa dini ambao wamepangwa kuwatetea mafisadi na kuishambulia familia ya Kikwete, ni janja ya kuwatangulia mbele ili wakisema jambo, wananchi waambiwe: “Si tulisema, mnaona sasa!?”

Hata hivyo, inafahamika kuwa makundi haya matatu ndiyo yako mstari wa mbele kupinga ufisadi na udini unaosambazwa na Kikwete na watu wake, hivyo lolote litakalosemwa halitakuwa geni; bali ni muendelezo unaofahamika. Pengine CCM haijui kuwa wananchi wanajua kinachoendelea. (WaTanzania are not stupid, ofcourse they know what is going on. You writing this piece betting on fact that WaTanzania hatujui kinachoendelea. You are betting on our ignorance)

Wagombea wa Kikwete 2015

Kwa kufuatilia mambo ya kisiasa yanavyokwenda na jinsi Rais Kikwete anavyoendesha mambo yake, kuna majina mawili ya watu wanaotajwa ambao angependa wachukue urais na umakamu wa rais wa Muungano mwaka 2015. Hii inatokana pia na imani yake kwamba Katiba mpya haitabadili mfumo wa sasa. (Now you can also predict people’s beliefs. Sources mzee, at least one source to come on the record. How can we believe u)

Sababu kubwa ni mbili: Kwanza, kutekeleza ahadi yake ya siri kwamba hawezi kuacha nchi kwa Mkristo (This is very dangerous. You are being irresponsible with your words throwing allegations like this one. SOURCES??) na pili, kuhakikisha uongozi mpya unamlinda yeye na familia yake dhidi ya misukosuko ya hapa na pale ambayo kawaida kote duniani hutokea mtu akishaacha urais. Hakika, naye hatapenda kushambuliwa kama inavyotokea kwa Mkapa.
Baada ya kufanikiwa kuwaengua pembeni Lowassa na Membe (Prof. Mwandosya kanusurika?) ni nani, basi, ambaye Kikwete anamtaka kwa urais wa 2015 na atachezaje karata zake kuhakikisha jina la mtu huyo linapeta?

Ili watu hao wawili anaowataka wakubalike, inaaminika kuwa Kikwete atatumia mtindo ule ule wa funika kombe mwanaharamu apite. Atawapendekeza kwa kutumia vigezo vinavyoficha ukweli (Now umekuwa Mnajimu. You can predict the future). Kutokana na hali ya kisiasa itakavyokuwa, anaweza kusema: “Jamani ni zamu ya wanawake sasa, tusitawale akina baba tu, nchi yetu wote.”

Iwapo wazo hili litakwama, basi, Kikwete anaweza kusema hivi: “Jamani sasa wenzetu wa Zanzibar nao, miaka 20 imepita, tuwape nao nafasi jamani.” Msemo huu, hata hivyo, hauna mashiko iwapo Katiba haitakuwa na agizo hilo; kwani upande wa Upinzani unaweza kuweka wagombea wote wa Bara.

Mbinu hiyo Kikwete ameshawahi kuitumia kwenye kujaza nafasi ya Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana ambapo alimpendekeza kijana wa Visiwani, na pia aliitumia kwenye kupata jina la mgombea wa uspika. Anaamini kuwa mbinu hiyo itasaidia kufunika hoja yake ya udini isionekane, na hivyo kufanikisha kupata rais Mwislamu.

Asha-Rose Migiro na Dk. Mwinyi

Katika miaka ya karibuni Kikwete amekuwa na mahusiano ya karibu ya kikazi na mwanamama mmoja ambaye kila baada ya miezi michache hufika Ikulu, na kisha picha nyingi hupigwa kuonesha kwamba wawili hao wanaelewana na wanashirikiana kisiasa pia.

Huyu ni mwanamama ambaye ni mmoja wa wanasiasa wachanga waliofaidika na vyeo vya uwaziri wa Kikwete mwaka 2005. Aidha, pale Tanzania ilipopewa mwanya wa kutoa jina la mwanamke wa kushika nafasi ya juu kimataifa, Kikwete hakusita kumtaja mwanamama huyu.
Nafasi hii ilikuwa baada ya Tanzania kufanya kampeni kubwa barani Afrika kuunga mkono jina la Waziri wa Mambo ya Nje wa Korea Kusini, Ban ki-Moon, kwenye kugombea nafasi ya ukatibu mkuu wa Umoja wa Mataifa.

Mwanamama huyo pia ana kisomo kizuri kinachokubalika na kinachoweza kuwaaminisha watu wanaotaka kuuliza maswali kuhusu uwezo wake kiutendaji wa kuiongoza nchi yenye matatizo ya uchumi na yenye mipasuko kibao kama Tanzania. Mwanamama huyo ni Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Dkt. Asha-Rose Migiro ambaye anaelezwa kuanza kujiandaa kurejea nyumbani Tanzania siku si nyingi.

Kwa upande wa Zanzibar, ni waziri mmoja kijana ambaye urafiki wake na Kikwete huwashangaza viongozi wengine wa Zanzibar; mathalani jinsi wanavyosalimiana kama watoto wa mjini. Katika mtandao wa YouTube Watanzania waliweka picha ya video ya Kikwete akisalimiana ‘kishkaji’ na waziri huyu kwenye Uwanja wa Amani, Zanzibar siku ya Januari 12, mwaka huu. Picha hiyo iliibua gumzo kubwa (What is your point?? What do u want us readers to take away from this useless paragraph? President and his minister wanasilimiana kishkaji, so what?)
Hivi karibuni Waziri huyu alipokabiliwa na msukosuko wa kutakiwa na wananchi kwamba ajiuzulu ambao kimsingi ulisababishwa na utendaji dhaifu wa Jeshi la Wananchi uliochukua maisha ya watu kwenye milipuko ya maghala ya silaha, alikataa na Kikwete hakusema kitu. Huyu ni Waziri wa Ulinzi, Dkt. Hussein Mwinyi.

Hitimisho langu

Inaaminika kuwa hao wawili ndio chaguo la Kikwete katika mbio za urais za 2015, na chaguo lake hilo linachagizwa zaidi na dini zao (How did you arrive to this conclusion? Throughout this piece, you have not convince us readers to buy on your accusation that our President is a religious fanatic) badala ya vigezo vya jumla vya sifa ambazo Watanzania wote tunataka mtu anayetaka kuwania urais kuwa nazo.

Hata hivyo, napenda nieleweke kwamba sina tatizo na rais ajaye kuwa Mwislamu au Mkristo; ilimradi tu awe ni kiongozi hodari, mchapakazi, mwadilifu na mwona mbali. Angalizo langu ni kwamba rais huyo ajaye asitafutwe kwa msingi wa dini yake; bali kwa vigezo hivyo vya ubora.
Nasisitiza hivyo; maana Watanzania katika ujumla wao hawajali dini ya mtu ila uadilifu na uchapakazi tu, lakini viongozi wetu ndio wenye matatizo ya udini. Na kwa hakika, Kikwete analo tatizo hilo.

Nihitimishe kwa kusisitiza kwamba wajibu wa wana-CCM ni kukisafisha chama chao kwa uaminifu na werevu, na kisha kuachia demokrasia iamue nani awe mgombea wa CCM mwaka 2015. CCM na Kikwete wawe waangalifu na dhana hii ya “sasa ni zamu yetu kutawala” ili Tanzania isitumbukie kwenye matatizo yanayosikika kwenye nchi zingine.
*************************************************************************************
The author and the publisher are being irresponsible and do not take their role in our society seriously. The piece has absolutely no standards to be published and consumed by our society. We are a democracy, but for democracy to work, a people have to be informed--otherwise we will continue to elect useless leaders. But our people can not be informed, if we keep on consuming garbage articles like this one.

Everybody can write, but to publish is a privilege that should be taken seriously.

3 comments:

January Makamba said...

I think the author knows exactly what he is doing. In politics, we call this a "hit job" and we really do not bother much thinking about.

Anonymous said...

The article is in Kiswahili ila maswali na hoja zako ziko kwa kiingereza,je lugha hauwezi?Walengwa wako si watakua watu wanaojua kusoma kiswahili?Naona ingekua vyema ungejibu, au kuuliza maswali hayo,kwa lugha iliyotumiwa na mwandishi.

Asante,

Mandala

bia said...

stori nzuri ila mwandishi ametumia lugha mbili tofaoti,hivyo amepunguza uzuri wa stori...ila mwandishi nae ana udini...ila jibu ni 2015..ahsante.