Friday, November 28, 2008

Language in this Blog

Watu kadhaa wamenitumia email kuuliza kwanini natumia Kiingereza kuandika kwenye blog hii wakati "lugha ya taifa" ni Kiswahili. Concept ya "lugha ya taifa" tunaweza kuijadili hadi asubuhi. Kwa kifupi, hapa ni ruksa kutumia Kiswahili au Kiingereza. Binafsi napenda kutumia Kiingereza kwasababu nadhani Kiswahili nakifahamu chote ila Kiingereza ni lugha ngeni kwangu kwahiyo napenda kuifanyia mazoezi zaidi lugha hii ngeni. And the only way to acquire proficiency kwenye lugha ni kuitumia mara kwa mara. 

And my sense ni kwamba mtu yoyote ambaye ameweza ku-navigate the web mpaka akafika kwenye blog hii certainly atakuwa anaelewe lugha ya Kiingereza. 

8 comments:

Unknown said...

Bwana mwandishi, kwanza asenta kwa kuweka topic hii hewani. Pili,kuna vitu sijakuelewa. Unaposema "concept ya lugha ya taifa tunaweza kuijadili mpaka asubuhi" unamaanisha nini? Tatu, ni kweli kuwa kufanya mazoezi ya lugha kunaboresha uwezo wa mtumiaji wa lugha, lakini wewe kama mwandishi unapaswa pia kutambua kuwa kuna wanaotembelea blog hii toka nje ya nchi ambao wakirudi nyumbani baada ya kusikiliza lugha za kigeni siku nzima wanawasha computer kusoma maandishi ya kiswahili-ili tu kupumzisha mawazo. Sasa hapa kwenye hili jamvi la taifaletu kila tukifungua tunakuta kama vile bado hatujafika "bongo". Ushauri tu ni kwamba hii inaweza kupunguza wateja wa jamvi hili, hasahasa walio nje ya nchi.

January Makamba said...

Ndugu Imani,

Nakushukuru kwa mchango. Inawezekana ukawa sahihi, kwamba wasomaji wengine wangependa kusoma posts za Kiswahili baada ya kuongea Kiingereza kutwa nzima. Nitazingatia ushauri wako bila kupoteza haja ya mimi nami niliyeko Bongo ambaye sina kabisa opportunities za kufanya mazoezi ya Kiingereza.

Unknown said...

sawasawa,asante kwa kutoa nafasi kwa lugha ya kiswahili.

Fadhy Mtanga said...

Wanakijiji wenzangu,
Nadhani ni jambo zuri sana kutokana uotaji wa magazeti tando kwa kasi kama uyoga.
Binafsi ninafurahia sana mapinduzi haya. Mapinduzi haya yametoa nafasi kwa watu wasio na pahala pa kusemea, wapate kusema.
Nakupongeza sana bw. Januari kwa kuwa na gazeti tando lako. Suala la lugha ipi unatumia ni la mapenzi yako binafsi.
Lililo muhimu kwetu wanakijiji wenzako ni mchango wako kifikra, ambao naamini ni muhimu zaidi kuliko lugha unayoitumia.
Lakini sisi kama Watanzania tungepata faraja sana kuona lugha yetu inakuzwa na maendeleo haya ya teknolojia.
Ni hayo tu kaka, ukipata wasaa karibu sana kijijini kwangu, kuna mashairi.
Kazi njema.

Anonymous said...

I just come accross your blog, while nazurura around Michuzi/Mjengwa blog.

Myself, I have been facing the same situation where to me, Swahili is my mother tongue, but unfortunately for more obvious reason and my own personal needs as a global Citizen, English has become my second language and I feel a first and MOST PRIORITY IN PERFECTING it through writing and talking.

But WHY THAT ???? In other words WHY making it MORE IMPORTANTLY THAN our own language ?? To me the answer lies by looking at educational history and looking where we are comming from and where we are going as a nation in this very competitive and small world, in between those timeline lie a range of important reasons to this answer, it will be unfair for me to go one by one.

But, Hey I wish Swahili could have been looked at the same PRISM, I guess we all know the answer to that!

And YES I DO LOVE KISWHAHILI, and I would make an extra effort passing that to my kids, if I continue living in this country, which I am now! THE PRIORITY KEEP CHANGING DEPENDS ON MY GLOBAL POSITIONING! Ha ha!
Thats true though, when you think about!

By Mchangiaji

Fadhy Mtanga said...

Bw ama Bibi Mchangiaji nimefurahi sana kusoma maoni yako kuhusu lugha ya gazeti tando la Bw Januari.
Kama nilivyopata kuchangia hapo awali, suala la lugha ni la mtu binafsi.
Nakubaliana na uamuzi wako wa kukipa Kingereza kipaumbele. Lakini siamini uhuru wa kuandika chochote katika magazeti tando yetu, unatupa pia uhuru wa kutozingatia sarufi katika maandishi yetu. Nina mashaka na sentensi,"where we are comming"
na nyingine, "in between those timeline lie a range of important reasons to this answer."
Mi si mjuvi wa lugha hiyo ya watu, lakini sentensi hizi mbili kama mfano, zinanifanya nihisi mashaka ya kisarufi.
Lakini nayathamini mawazo yako.
Idumu lugha yetu adhimu ya Kiswahili. Ni hayo tu.

Anonymous said...

Fadhy Mtanga, nimefurahi na maoni yako. Wasi wasi mkubwa pale ninapoandika kitu chochote ikiwa kwa lugha nyengine au lugha asilia ikawa ni vigumu kwa wengine kukielewa.

Hata hivyo, imeonyesha yale maudhii niliyoyasema katika hayo maoni yangu hapo juu yameeleweka, na HILO NDILO MUHIMU KWANGU NA KWAKO, hapo MARIDHAA YANGU YANAKUWA YAMEKAMILIKA.

Hata hivyo ningefurahi kama ungeweza kunisawazisha kwa kile nilichokitolea dondozi, yaani kwa kumaanisha ufahamu pepe wa ile sentensi ya kiingireza niliyoikosea. Je ni muundo wa sentence asilia ni mbaya ? au maneno hayako katika mfumo sahihi wa kile ninachokisema. Nitafurahi kwa mchango wako, vile vile ni lazima uwe ni ufahamu mbinu, kwa msingi mzima wa mitandao huria (blogging), hii inaniweza mimi au wewe au mwananchi mwenza kuweza kutoa dodosi zao huria, bila ya kuwa na vipingamizi vya mkondo mkubwa wa habari huria (yaani mainstream media), kama ulivyojieleza katika maoni yako awali. Kwa hiyo basi na mimi ni mmoja wa hao wadodosi HURIA. Never been perfect yet quest for PERFECTION, unless ningekua nafanya kazi New York Times. Sijui umenifahamu kiini cha maudhii yangu, yapi ninayokusudia.

Hata hivyo shukrani, kwa maoni na ndiyo sababu kubwa ambayo mimi binafsi kama mchangiaji kutoa maudhui yangu kwa lugha ya kiingereza yote ni kujaribu kujiboresha na kuweza kukukuza uwezo wangu wa kusema na kuandika lugha hiyo.

Hata hivyo nimetembelea mtandao wako, mashairi yako yamesimama, asante kwa udondozi wako.

Shukran

Ni mimi Mchangiaji.

Fadhy Mtanga said...

Mchangiaji,
Nimefurahi sana kuona umepita tena na kuweka maoni yako. Hii ndiyo raha ya blog.
Nakushukuru sana kwa kuwa umenipa somo zuri baada ya mimi kutoa maoni yangu. Ni kweli huu ni uhuru mzuri zaidi katika kupashana habari. Kila mtu anatoa maoni yake kadri ya uwezo wake na kwa lugha aipendayo. Kuna mtu aliwahi weka maoni yake kwenye blog yangu kwa Kifaransa. Sikukielewa, lakini niliamini kuwa alitoa mchango wa thamani.
Pia napenda kukushukuru sana kwa kuzuru blog yangu. Nakukaribisha sana ndugu. Tafadhali usiache kuchangia maoni yako kwa yale ninayoyaandika.
Kwa pamoja tunajenga, tunasonga mbele daima.
Kwa mara nyingine, nakushukuru sana na karibu sana.
Kazi njema.