Wednesday, November 15, 2017

Tanzania Tanzania
Tanzania Tanzania
Nakupenda kwa moyo wote
Nchi yangu Tanzania
Jina lako ni tamu sana
Nilalapo nakuota wewe
Niamkapo ni heri mama wee
Tanzania Tanzania
Nakupenda kwa moyo wote

Tanzania Tanzania
Ninapokwenda safarini
Kutazama maajabu Biashara nayo makazi
Sitaweza kusahau mimi mambo mema ya kwetu kabisa
Tanzania Tanzania
Nakupenda kwa moyo wote

Tanzania Tanzania
Watu wako ni wema sana
Nchi nyingi za kuota nuru yako hakuna tena
Na wageni wa kukimbilia ngome yako imara kweli wee
Tanzania Tanzania
Heri yako kwa mataifa

Tanzania Tanzania
Karibu wasio na kwao
Wenye shida na taabu
Hukimbizwa na walo wezi
Tanzania yawakaribisha
Tuungane kiume chema wee
Tanzania Tanzania
Mola awe na we daima